Timu za EPL kuwakosa wachezaji watakaoshiriki AFCON

Dismas Otuke
2 Min Read

Makala ya 34 ya fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika AFCON yataandaliwa nchini Ivory Coast kati ya Januari 13 na Februari 11 mwaka ujao wa 2024.

Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu Uingereza vinatarajiwa kukosa huduma za wanandinga watakaoshiriki kindumbwendumbwe hicho.

Arsenal itakosa huduma za Mohamed Elneny wa Misri na Thomas Partey wa Ghana huku Chelsea ikimkosa Nicolas Jackson wa Senegal wakati Liverpool ikimpoteza
Mohamed Salah wa Misri.

Manchester United watawapoteza Andre Onana wa Cameroon ,Amad Diallo wa Ivory Coast, Hannibal Mejbri wa Tunisi na Sofyan Amrabat wa Morocco.

Tottenham Hotspur itamkosa Yves Bissouma wa Mali na Pape Matar Sarr wa Senegal huku West Ham United ikikosa huduma za Mohammed Kudus wa Ghana, Said Benrahma wa Algeria , Maxwel Cornet wa Ivory Coast,na Nayef Aguerd wa Morocco.

Fulham itakosa wachezaji Calvin Bassey, Alex Iwobi wa Nigeria na Fode Ballo-Toure wa Senegal.

Brentford itawapoteza Frank Onyeka wa Nigeria, Bryan Mbeumo wa Cameroon na Yoane Wissa wa DR Congo.

Crystal Palace itawakosa Jordan Ayew, Jeffrey Schlupp wote wa Ghan na Cheick Doucoure wa Mali huku Brighton & Hove Albion ikikosa huduma za Tariq Lamptey wa Ghana , Carlos Baleba wa Cameroon, na Simon Adingra wa Ivory Coast).

Aston Villa itampoteza Bertrand Traore wa Burkina Faso ,Nottingham Forest iwakose Ola Aina, Taiwo Awoniyi wa Nigeria, Serge Aurier, Willy Boly, Ibrahim Sangare wote wa Ivory Coast, Moussa Niakhate, Cheikhou Kouyate wote kutoka Senegal.

Wolverhampton Wanderers wanatarajiwa kuwakosa Rayan Ait-Nouri wa Algeri na Boubacar Traore wa Mali huku Everton ikimpoteza Idrissa Gueye wa Senegal.

Website |  + posts
Share This Article