Timu ya Kenya Simbaz yaandaa mazoezi Kakamega

Marion Bosire
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande, maarufu kama “Kenya Simba,” imekita kambi katika Kaunti ya Kakamega kwa maandalizi ya mechi ya Elgon Cup dhidi ya timu ya taifa ya Uganda.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Jerome Paarwaters, amesema walichagua Kakamega kwa mazoezi kutokana na utulivu wa mazingira na pia kwa kuwa asilimia kubwa ya wachezaji ni kutoka klabu ya Kabras RFC ambayo ina mizizi katika eneo hilo.

Nahodha wa Simba, George Nyambua, amesema kuwa timu iko tayari kukabiliana na wapinzani wao, Uganda, na amewataka mashabiki kutarajia ushindi.

Aidha, wachezaji hao walipata fursa ya kutembelea kiwanda cha sukari cha West Kenya ambacho kinadhamini klabu ya Kabras Sugar RFC.

Share This Article