Takriban tiketi 20,000 za derby ya Mashemeji Jumapili hii kati ya AFC Leopards na Gor Mahia zinatarajiwa kuuzwa.
Kulingana na Leopards ambao ni wenyeji wa mechi hiyo wananuia kuuza tiketi 18,000 za maeneo ya kawaida, kwa ada ya shilingi 300 kila moja.
Tiketi 1,800 za jukwaa kuu zinauzwa kwa shilingi 1,000, na tiketi 80 za eneo la VVIP zikiuzwa kwa shilingi 5,000 kila moja.
Mashabiki wamehimizwa kununua tiketi zao mapema kabla ya siku ya mechi .
Mechi hiyo itaandaliwa Jumapili hii katika uwanja wa taifa wa Nyayo kuanzia saa kumi alasiri.
Itakuwa mara ya kwanza katika msimu huu wa Ligi Kuu ya FKF, kwa derby hiyo kuchezwa baada ya kuahirishwa mara mbili.