Jumapili Oktoba 29, 2023, awamu ya tatu ya tamasha ya mihogo iliandaliwa katika ufuo wa Coco, mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania.
Katika tamasha hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2021, mihogo huandaliwa na kupakuliwa kwa njia tofauti.
Huwa inasheheni burudani kutoka kwa wanamuziki, soka ya ufuoni, mashindano ya kula mihogo kati ya mambo mengine mengi.
Wadhamini wa tamasha hiyo ni pamoja na kampuni ya vinywaji ya Cocacola, kampuni ya mawasiliano ya Clouds Media na wengine wengi.
Reuben Ndege afisa ambaye anasimamia ubunifu na mikakati katika kampuni ya Clouds Media ndiye mwanzilishi wa tamasha hiyo ya mihogo.
Alisema nia yake ilikuwa kuhimiza vijana kujihusisha na biashara ya mihogo kuanzia shambani hadi mezani.