Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza nyongeza ya asilimia 35.1, kwa wafanyikazi wa serikali wanaopokea mishahara ya chini .
Akitangaza hayo wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya wafanyikazi leo Rais Samia, amesema hii ni kufuatia kuongezeka kwa pato la taifa hilo kutokana na juhudi za wafanyikazi.
Samia amesema nyongeza hiyo itaanza kutekelezwa Julai mosi mwaka huu, huku wafanyikazi wa mishahara ya chini zaidi wakitarajiwa kupokea mishahara mipya ya 500,000 kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 370,000.
Kiwango hicho ni sawia na shilingi 31,000 kutoka 23,000 za Kenya kwa kila mwezi.
Rais Samia pia ameahidi kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa viwango vingine kulingana na jinsi uchumi utakavyoimarika.