Takwimu za kipute cha CHAN kufikia sasa

Wenyeji wenza Tanzania wanaongoza kundi B kwa alama 6, wakifuatwa na Burkina Faso kwa alama 3.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya mechi 10 zimechezwa tangu kuanza kwa makala ya nane ya fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN.

Fainali hizo zinaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania na zilianza Agosti 2.

Magoli 18 yamefungwa likiwemo moja la kujifunga pamoja na kadi nyekundu kutolewa.

Morocco wanaongoza kundi A kwa alama 3 sawa na Kenya.

Wenyeji wenza Tanzania wanaongoza kundi B kwa alama 6, wakifuatwa na Burkina Faso kwa alama 3.

Algeria waliomaliza nafasi ya pili mwaka 2022, wanaongoza kundi C kwa alama 3 sawia na Guinea.

Mabingwa watetezi Senegal wanaongoza kundi D kwa pointi 3, wakifuatwa na Congo na Sudan kwa alama 1 kila moja.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article