Takriban watu 100 wafariki kutokana na mafuriko Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Takriban watu 100 wameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko yanayosababishwa, na mvua kubwa inayoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.

Miili sita iliopolewa katika mto ulio eneo la Sultan Hamud siku ya Jumamosi, kufuatia kusombwa kwa lori walilokuwa wakisafiria Ijumaa.

Pia shughuli ya kutafuta miili zaidi inaendelea katika mto wa Mathare, baada ya mvua kusomba nyumba wiki iliyopita.

Mafuriko yameripotiwa katika maeneo mengine nchini ikiwemo Mwiki, huku shirika la World Vision likitoa mchango wa shili gi elfi kumi kwa kila familia iliyoathiriwa mtaani Mathare.

Haya yanajiri huku watabiri wa haki ya anga wakionya kuendelea kwa mvua ya masika, na kuwatahadhari wanaoishi karibu na maeneo hatari kuhama.

Website |  + posts
Share This Article