Taasisi za Kenya zahimizwa kuwaajiri makarani waliohitimu

Tom Mathinji
1 Min Read

Taasisi za umma na zile za kibinafsi zimehimizwa kutafuta huduma za makarani waliohitimu, kuhakikisha uongozi bora katika taasisi hizo.

Mwenyekiti wa taasisi ya makarani waliohitimu (ICS) Joshua Wambua na afisa mkuu mtendaji wa taasisi hiyo  Jeremiah karanja, walielezea umuhimu wa huduma za makarani waliohitimu katika ukuaji wa mashirika.

Wakizungumza wakati wa sherehe ya 12 ya tuzo za uongozi bora, wawili hao walisema taasisi ya ICS imezawadi mashirika kadhaa ya umma na zile za kibinafsi kwa kudhirisha uongozi wa kupigiwa mfano.

Wambua aliipongeza serikali kwa kushirikiana na taasisi ya ICS wakati wa hafla ya kuwaingiza kazi wenyeviti na wanachama wa bodi za usimamizi wa mashirika ya serikali kuhusu njia mwafaka za usimamizi.

Mbunge wa Rarieda Otiende Amolo ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo, aliipongeza taasisi ya ICS kwa kuwatambua watu wanaodhihirisha kiwango cha juu cha uongozi bora.

Share This Article