Katibu Mkuu wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Edwin Sifuna, amesimama kidete kuwa kamwe hatahudumu katika wadhfa huo chini ya kiongozi mpya aliyeidhinishwa jana Oburu Odinga na kongamano maalum la wajumbe (SNDC).
Sifuna aliyesema haya Ijumaa alipoandaa mkutano sambamba na ule wa kundi la Oburu.
Oburu aliwataka wanachama wengine wa ODM walio na maoni kinzani kutumia mbinu za kutatua migogoro zilizo chamani badala ya kuanika tofauti zao hadharani.
Kauli ya Seneta wa Nairobi inaongeza joto ndani ya chama hicho mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.