Steve Munyakho hatimaye awasili nyumbani

Tom Mathinji
1 Min Read
Steve Munyakho awasili nyumbani.

Steve Munyakho, raia wa Kenya mwenye umri wa miaka  51, aliyeachiliwa huru baada ya kuhukumiwa kifo nchini Saudi Arabia, aliwasili nchini Kenya Kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatatu usiku.

Munyakho, ambaye sasa amebadili jina na kuitwa Abdukareem, aliwasili kutoka Jeddah akiwa ameandamana na balozi wa Kenya nchini Saudi Arabia Mohammed Ruwange, na kulakiwa na mamake mzazi mwanahabari mkongwe Dorothy Kweyu na marafiki.

Wengine waliomlaki ni pamoja na Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje Korir Sing’Oei  na wanakamati wa kamati  iliyoshughulika kumrejesha nyumbani Steve.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili nchini, Steve alitaja kuachiliwa kwake kuwa “Miujiza”.

Kuwasili kwake nyumbani kunatamatisha ukurasa wa mahangaiko na mateso Kwa familia yake, ambayo kamwe haikukata tamaa licha ya masaibu yaliyomzingira Stevo.

“Nina Furaha kurejea nyumbani. Iwepo wangu hapa nchini ni miujiza. Nashukuru Allah kwa kunipa uhai,” alisema Munyakho.

Mamake aliishukuru serikali ya Kenya na Wakenya kwa jumla kwa msaada wao usio na kifani.

“Shukran sana balozi Mohamed Ramadhan Ruwange, kwa kumwasilisha salama mwana wangu wa kwanza hapa nchini. Shukran sana Kwa watu wa Mungu kwa maombi na mchango wenu wa kifedha kwa Stevo,” alisema Dorothy Kweyu.

Website |  + posts
Share This Article