Starlets kumenyana na Ivory Coast Jumatano usiku

Tom Mathinji
1 Min Read
Timu ya taifa ya soka ya akina dada Harambee starlets.

Timu ya taifa ya soka ya akina dada Harambee Starlets, itapimana nguvu na Ivory Coast leo usiku katika mechi yao ya pili ya kirafiki katika uwanja wa Alassane Ouattara Ebimpé Olympic Stadium.

Starlets watatumia mechi hiyo kujinoa makali kwa mechi za kuwania ubingwa wa Kombe la Bara Afrika kwa akina dada, zinazotarajiwa kuanza Machi 17,2026 nchini Morocco.

Timu hiyo inayoongozwa na Beldine Odemba ya wachezaji 25, itakuwa makini kuandikisha ushindi baada ya kushindwa mabao 2-0 na Benin katika mechi yao ya kwanza ya kirafiki siku ya Jumatatu.

Harambee Starlets imetengwa katika kundi ‘A’ la fainali hizo za bara Afrika kwa akinadada pamoja na wenyeji Morocco, Algeria na Senegal na itaanza mechi zake dhidi ya Morocco tarehe 17 mwezi huu, kisha icheze dhidi ya Senegal tarehe 20 na hatimaye Algeria siku tatu baadaye.

Timu hiyo ina wachezaji 12 wanaocheza soka bara ulaya, huku 13 wakitoka kwa timu za ligi za hapa nyumbani.

Starlets wanarejea kwa kinyang’anyiro hicho kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mara ya kwanza mwaka 2016.

 

Share This Article