Starlets wafunga safari kurejea nyumbani kutoka Ivory Coast

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets, imelazimika kukatiza mazoezi yao na kurejea nyumbani kufuatia kuahirishwa kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON).

Starlets walikuwa wamecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Benin na wenyeji Ivory Coast na kupoteza zote wiki hii, na walikuwa wafunge safari kuelekea Ufaransa kwa kambi ya mazoezi mjini Marseille.

Hatua ya kukatiza kwa mazoezi inafuatia tangazo la shirikisho la soka Afrika -CAF, kuahirisha michuano ya WAFCON kutoka Machi 17 hadi Aprili 3 hadi Julai 25 na Agosti 16 mwaka huu.

Kenya imejumuishwa kundi A pamoja na Morocco, Senegal na Algeria kwenye fainali za WAFCON.

Share This Article