Speed Darlington akamatwa tena, Burna Boy adaiwa kuhusika

Darlington alikamatwa Oktoba kwa madai ya kumchafulia Burna Boy jina

Marion Bosire
1 Min Read
Speed Darlington

Mwanamuziki wa Nigeria Speed Darlington amekamatwa tena na maafisa wa polisi katika eneo la Owerri, jimbo la Imo nchini Nigeria.

Wakili wake aitwaye Deji Adeyanju alitangaza hayo kupitia mtandao wa X akisema kwamba alikamatwa kwenye tamasha lake punde baada ya kurejea Nigeria.

“Mteja wetu Speed Darlington au ukipenda AKPI amekamatwa na maafisa wa polisi wa Nigeria huko Owerri kwenye tamasha lake baada yake kurejea nchini Nigeria.” alielezea Deji kwenye mtandao wa X.

Deji ambaye pia ni mwanaharakati, alimlaumu mwanamuziki Burna Boy kwa masaibu ya Darlington akishangaa ni kwa nini anamkandamiza ilhali ameimba nyimbo dhidi ya maovu kama hayo.

Mwezi Oktoba, Darlington alikamatwa na polisi jijini Lagos na akasafirishwa hadi Abuja ambako alizuiliwa.

Hatua hiyo ilifuatia maneno aliyomtupia Burna Boy kwenye video aliyochapisha huku akitilia shaka tuzo za Grammy za Burna Boy.

Alimhusisha Burna Boy na mwanamuziki wa Marekani anayekabiliwa na utata P Diddy ambaye anaripotiwa kuandaa hafla za kingono na kisha kufanikisha taaluma za wasanii.

Baadaye alichapisha taarifa kuhusu mafuta ya watoto na kisha kurekodi wimbo uitwao “Baby Oil” ambao aliimba jukwaani.

Wakati huo ilidhibitishwa kwamba Burna Boy ndiye alimshtaki mwanamuziki huyo kwa kile ambacho kilitajwa kuwa kumchafulia jina lakini baadaye aliachiliwa kwa dhamana.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *