Somalia yakataa upatanishi katika mzozo wake na Ethiopia

Tom Mathinji
1 Min Read

Somalia imesema hakuna nafasi ya upatanishi katika mzozo wake na Ethiopia iwapo taifa hilo halitajiondoa katika makubaliano yenye utata na eneo lililojitenga la Somaliland.

Mvutano katika eneo hilo la Pembe mwa Afrika, umeongezeka baada ya Ethiopia isiyo na bandari kuafikia makubaliano ya maelewano na eneo la Somaliland mnamo tarehe moja mwezi huu ambao unaipa fursa ya kuingia baharini.

Haya yanajiri baada ya mgogoro huo kujadiliwa na muungano wa Afrika siku ya Jumatano, huku nchi hizo mbili zikitakiwa kudumisha utulivu wakati ambapo suluhu la amani linatafuwa.

Shirika la IGAD pia lilifanya mkutano nchini Uganda siku ya Alhamisi, kuhusiana na mzozo huo wa Ethiopia na Somalia..

Website |  + posts
Share This Article