Mabingwa wa Ligi kuu nchini Kenya mwaka 2009 Klabu ya SOFAPAKA, watachuana na Naivas FC katika, mechi ya mchujo kuwania nafasi moja iliyosalia kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Naivas watawaalika Sofapaka Julai 6 katika uwanja wa Kenyatta kaunti ya Machakos, kabla ya marudio kuchezwa Julai 14 uwanjani humo SOFAPAKA ikiwa mwenyeji .
Mshindi wa jumla wa mchuano huo atashiriki Ligi Kuu msimu ujao.
SOFAPAKA maarufu kama ‘Batoto ba Mungu’ walimaliza katika nafasi ya 16 katika Ligi Kuu ya FKF.
Upande wao Naivas FC walifuzu kwa mchujo huo, baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi ya NSL.
Tayari timu za Mara Sugar na Mathare United zimepandishwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao baada ya kutwaa nafasi mbili za kwanza.