Simba wadinda kulala chali nyumbani Dar dhidi ya Mwarabu

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka nchini Tanzania Simba Sports Club wamelazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Al Ahly ya Misri, katika duru ya kwanza ya robo fainali ligi ya soka Afrika.

Wageni Ahly ukipenda mashetani wekundu walichukua uongozi dakika ya za mwisho kipindi cha kwanza kupitia kwa Radi Slim .

Kipindi cha pili mnyama Simba alikuja kwa matao ya juu na Dennis Kibu na Sadio Kanoute wakibusu nyavu za Mwarabu mara moja kila mmoja ndani ya dakika 6.

Hata hivyo uongozi wa wenyeji ulizimwa dakika tano baadaye, baada ya kiungo Kahraba kusawazishia wageni.

Mkwangurano huo ulisakatwa katika uwanja Benjamin Mkapa Ijumaa jioni na kushuhudiwa na mashabiki 60,000 wakiwemo vinara wakuu wa FIFA Gianni Infantino na viongozi wa CAF.

Marudio ni Jumatatu ugani Cairo huku mshindi wa jumla akitinga nusu fainali.

Share This Article