Simba wa Teranga kufungua kampeni dhidi ya nge wa Gambia AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Senegal maarufu kama Teranga Lions, watafungua hekaheka za kutetea kombe la AFCON dhidi ya limbukeni Gambia ukipenda the Scorpions Jumatatu jioni.

Senegal watamenyana na Gambia katika mechi ya kwanza ya kundi C kuanzia saa kumi na moja jioni katika uchanjaa wa Yamoussoukro.

Senegal ambao wanaongozwa na nyota wa zamani Alliou Cisse wanajivunia kuwa timu bora ya pili katika kipute cha mwaka huu nchini Ivory Coast, huku Gambia wakiorodheshwa wa mwisho miongoni mwa timu 24 zinazoshiriki.

Baadaye saa mbili usiku, itakuwa zamu ya Simba wasiotikisika wa Cameroon ukipenda Indomitable Lions, kukabana koo na tembo au Syli Nationale kutoka Guinea katika mkwangurano wa pili kundi B ikiwa derby ya Afrika Magharibi.

Hatimaye saa tano usiku, kundi C litafungua milango kwa mechi zake mbweha wa Algeria ukipenda The Foxes, wakipimana ubabe na swara kutoka Angola almaarufu Palancas Negras.

Mikwangurano yote itarushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.

Website |  + posts
Share This Article