Watani wa jadi Tanzania bara, Simba na Yanga watazindua uhasama Jumatano hii katika derby ya Kariakoo, kuwania Kombe la Muungano.
Mchuano huo utasakatwa kuanzia saa mbili na robo usiku wa Aprili 29, katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Mashindano hayo yanayoandaliwa kila mwaka yanashirikisha timu nane kutoka Tanzania bara na kisiwani Zanzibar.
Simba waliibwaga Mafunzo bao moja bila katika robo fainali, kabla ya kuwatema nje Mlandege 3-0, katika hatua ya nusu fainali.
Upande wao vijana wa Jangwani, Yanga, waliititiga Mwembe Makumbi City 4-0, katika kwota fainali,kabla ya kuwabandua Azam United 2-1, katika nusu fainali.