Gachagua afika Mahakamani,ataka alipwe ridhaa

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, amefika  katika Mahakama Kuu ya Milimani mapema Jumatatu, kushuhudia kuanza kuskizwa kwa kesi yake ya  kufurushwa afisini.

Hata hivyo Gachagua amesema anataka analipwe ridhaa badala ya kurejeshwa afisini alivyokuwa ametaka awali.

Kiongozi huyo wa chama cha DCP alikuwa amepinga kutimuliwa kwake afisini kwa njia isiyo halali, akitaka Mahakama Kuu, kuharamisha hatua ya bunge la kitaifa kumbandua na kutaka arejeshwe afisini.

Hata hivyo katika maombi mapya ya kesi hiyo Gachagua anataka Mahakama Kuu, iharamishe kufurushwa kwake na alipwe ridhaa kwa hasara aliyopata .

Gachagua aliandamana na mawakili wake na wandani wake wa upinzani wakiwemo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka,kiongozi wa chama cha DAP -K, Eugene Wamalwa ,familia yake , Millicent Omanga na Seneta wa  Nyandarua John Methu .

Paul Muite anaongoza jopo la Mawakili wa Gachagua ambalo pia linawajumuisha Elisha Ongoya na  Ndegwa Njiru.

Kesi hiyo inasikizwa na Majaji Erick Ogolla, Anthony Mrima, na  Freda Mugambi.

Share This Article