Mwajentina Tello Facundo kusimamia mechi kati ya Ufaransa na Morocco

Pambano hilo la Kombe la Dunia litarushwa mubashara kupitia runinga ya kitaifa ya KBC Channel 1 kuanzia saa tano usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwajentina Tello Facundo atakuwa refa wa Kati kati ya uwanja wakati wa robo fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Morocco leo Alhamisi usiku.

Facundo atasaidiwa na Juan Pablo Belatti na Gabriel Chade, wote kutoka Argentina kama wasaidizi wa kwanza na wa pili mtawalia.

Darío Herrero atakuwa afisa wa nne huku Cristian Navarro akiwa refa msaidizi wa akiba.

Pambano hilo litarushwa mubashara kupitia runinga ya kitaifa ya KBC Channel 1 kuanzia saa tano usiku.

Share This Article