Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaonya wanaharakati kwa matendo yao ya kigaidi.
Samia amesema kundi hili la watu huwa linatumia njia ya uanaharakati kujitambulisha duniani lakini ni wenye nia tofauti kulingana na matendo yao.
“Watu au kundi hilo linakuwa na kauli zinazovaa sura ya kizalendo lakini kwa undani ni maslahi binafsi,” amesema Rais Samia.
Amewakosoa wanaharakati kwa kutegemea vurugu ili kuendesha maisha yao kwa maslahi ya wengine.
“Niwaonye wale wote wanaojishuhulisha na vitendo hivyo, kwamba taifa lolote duniani hutumia nguvu ya dola kuhami raia wake na kulinda heshima yake,” amesema Rais Samia.
Rais Samia ameonyesha kuwa tofauti zimekuwepo lakini sio kwa nia ya kubomoa wala uvunjifu wa amani.
Aidha, amesihi Tanzania kushikamana kwa ajili ya taifa wala sio kulidhalilisha kwa sababu ya matwaka ya watu binafsi.
Rais Samia amewahikikishia raia kuwa serikali iko imara kuwalinda pamoja na mali zao.
Taarifa ya BBC