Miamba wa Afrika, Morocco wamepatwa na pigo kwa robo fainali ya Kombe la Dunia Alhamisi usiku kiwarani Boston dhidi ya Ufaransa baada ya kiungo wao Ismael Saibari kuthibitishwa kukosa mechi hiyo kutokana na jeraha.
Saibari alijeruhiwa na kuondolewa uwanjani katika mechi ya raundi ya 16 bora dhidi ya Canada.
Kocha Mohamed Ouahbi amethibitisha kuwa Saibari atakosa mechi ya kwota fainali kwani hajapona jeraha.
Saibari, aliye na umri wa miaka 25, alifunga bao moja dhidi ya Brazil, dhidi ya Scotland na dhidi ya Haiti, akiwa mwanandinga wa kwanza wa Afrika kufunga bao katika mechi tatu mtawalia za Kombe la Dunia.
Kiungo huyo mshambulizi amesaini mkataba na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, kutoka PSV ya Uholanzi.
Soufiane Rahimi anatarajiwa kuchukua nafasi ya Saibari, huku pia Hakim Ziyech akitarajiwa kujumuishwa kikosini.
Morocco watamenyana na Ufaransa katika uwanja wa Boston leo usiku katika mechi ya robo fainali.