Ni afueni kwa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna baada ya jopo la kutatua migogoro ya vyama vya kisiasa kuharamisha kufurushwa kwake kama Katibu Mkuu wa chama cha ODM.
Katika uamuzi huo wa siku ya Alhamisi, jopo hilo lilipinga kutimuliwa kwa Sifuna, lakini badala yake likaidhinisha mkutano maalum wa wajumbe kuandaliwa hii leo Ijumaa.
Katika kupiga breki kutimuliwa kwa Sifuna, jopo hilo lilisema kuwa chama hakikutumia mbinu mbadala za kuwaadhibu wanachama kabla kuafikia kumtimua.
Ulikuwa ushindi pia kwa kaimu kiongozi wa chama cha ODM Oburu Oginga baada ya jopo kumtambua kama mwenyekiti halali wa chama.