Zaidi ya shule 150 za kibinafsi nchini Kenya zitanufaika na gesi ya kupikia baada ya shirika la MyCredit kusaini mkataba na kampauni ya mafuta nchini Uganda ya Volcanova Energy Africa .
Katika makubaliano hayo MyCredit imetoa kitita cha shilingi nusu bilioini zitakazowezesha shule takriban 150 kuwekewa mitungi ya gesi ya kilo 1,000 ya kupikia kila moja, pamoja na sufuria za upishi kwenye jikoni hali inayotarajiwa kupunguza matumizi ya ukataji miti inayotumika kwa upishi .
Pia matumizi ya gesi ya kupikia yatapunguza uchafuzi wa mazingira na athari ya moshi kwa wanafunzi ,wapishi na pia kupunguza ukataji miti.
Meneja Mkurugenzi wa MyCredit Wangaruro Mbira, alisema kando na mpango huo wanahimiza shule kupanda miche ya miti na kukidhia ile iliyokatwa kwa ajili ya kuni.
Upande wake Afisa Mkuu mtendaji wa Volcanova Energy Yusuf Ssemakula, alifichua kuwa mpango huo tayari umefanikiwa nchini Uganda na kwa sasa shule za umma zimeshirikishwa.
Aidha,shule hizo zinatarajia kupunguza bajeti zinazotumia kwa mapishi ya vyakula vya wanafunzi na hivyo kuongeza faida.
Mradi huo ulizunduliwa katika shule ya Fadhili Junior mtaani Umoja kaunti ya Nairobiu, huku lengo likiwa kujumuisha shule zipatazo 1,000 kote nchini ifikiapo mwaka ujao.