Serikali kamwe haitongeza muda wa kandarasi zilizopo katika Mamlaka ya Afya ya Umma, SHA punde muda wa mikataba ya sasa utakapokamilika tarehe 14 mwezi huu.
Haya yameafikiwa Jumatatu kati ya waziri wa Afya Aden Duale na kamati ya Afya katika baraza la Magavana nchini CoG.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa kamati ya afya katika COG ambaye pia ni Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir na Duale, pia iliafikiwa kuanzishwa kwa mchakato wa kusaini kandarasi mpya za hospitali zitakazotoa huduma za matibabu baina ya mwaka 2026 na 2029.
Hata hivyo, serikali imetoa hakikisho la kukamilisha utoaji kandarasi kwa wakati ufaao ili kuhakikisha wagonjwa wanapokea huduma za matibabu bila tatizo lolote.
Kikao hicho pia kimeshirikisha maafisa wa SHA, Shirika la Afya ya Digitali (DHA) na wasimamizi wa utoaji huduma za matibabu ili kutekeleza mikataba mipya ya miaka mitatu ijayo.
Kulingana na mpangilio huo, hospitali na vituo vya afya vya viwango vya Level 4 au Level 5 vitatoa tu huduma zilizoidhishwa.