Juhudi zaimarishwa kurejesha Mfumo Ikolojia wa Cherangany

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, ametangaza mpango wa miaka kumi unaolenga kurejesha mfumo ikolojia wa milima ya Cherangany, ili kuokoa maisha na rasilimali hiyo muhimu.

Kulingana na Murkomen, mfumo ikolojia wa milima ya Cherangany umeharibiwa na shughuli haramu za kibinadamu na kusababisha maisha, bioanuwai na maporomoko ya kila mara ya udongo.

“Asilimia 15 ya mfumo ikolojia wa milima ya Cherangany imeharibiwa kabisa, huku asilimia 67 ikiharibiwa kwa kiwango. Hekari 41,547 ya msitu na hekari 76,757 ya eneo la nyasi imeharibiwa,” alisema Murkomen.

Aliyasema hayo Ijumaa wakati wa mkutano wa washirika wa mpango wa urejeshaji wa mfumo ikolojia wa milima ya Cherangany katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet.

Murkomen alilaumu serikali zilizopita kwa uharibifu wa mfumo ikolojia wa eneo hilo uliojumuisha msitu wa Embobut.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Mazingira na Mbadiliko ya Tabianchi Dkt. Deborah Barasa, Gavana wa Elgeiyo Marakwet Wisley Rotich, na Seneta  William Kisang, wabunge na Makatibu wa Wizara miongoni mwa wenginr.

Share This Article