Ruto: Mageuzi katika kilimo yamezaa matunda

Uzalishaji mahindi kote nchini uliongezeka kutoka magunia milioni 44 mnamo mwaka 2022 hadi milioni 71 mwaka huu.

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumatano amehutubia taifa katika majengo ya bunge wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbalu nchini. 

Katika sekta ya kilimo, Rais Ruto amesema hadi sasa, magunia milioni 38.5 ya mbolea ya bei nafuu yamesambazwa kwa wakulima katika hatua ambayo imesaidia kuboresha uzalishaji wa mazao.

“Uzalishaji wa mahindi kote nchini uliongezeka kutoka magunia milioni 44 mnamo mwaka 2022 hadi milioni 71 mwaka huku mahindi yaliyoagizwa yakipungua kutoka magunia milioni 9.9 hadi milioni 3.3,” alisema Ruto kwenye hotuba yake ya nne kwa taifa kutoka bungeni tangu alipoingia madarakani mwaka 2022.

“Bei ya wastani ya kitaifa ya paketi ya kilo mbili ya unga ilipungua kutoka shilingi 230 mwezi Septemba mwaka 2022 hadi shilingi wastani wa shilingi 152 mwezi Septemba mwaka huu.”

Aliongeza kuwa mageuzi hayo pia yamezaa matunda katika sekta ya kahawa na majani chai huku wakulima wakifurahia mapato bora.

Ruto amesema serikali imedhamiria kuendelea kuboresha uzalishaji katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote kwa bei nafuu kote nchini.

 

 

Share This Article