Shujaa yaibuka kwa kishindo na kuzikomoa Canada na Ubelgiji

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande ilirejelea tambo za ushindi baada ya kuzisasambua Canada na Ubelgiji, katika msururu wa pili wa mashindano ya dunia ya HSBC daraja ya pili yanayoendelea nchini Uruguay.

Shujaa iliwaparakasa Ubelgiji alama 20-0, mapema Jumapili baada ya kuibwaga Canada pointi 19-5, Jumamosi usiku.

Awali vijana wa Kenya chini ya ukufunzi wa Kevin Wambua, waliambulia kipigo cha alama 10-14 dhidi ya Marekani Jumamosi usiku.

Kenya itarejea uwanjani leo usiku dhidi ya Ujerumani na hatimaye kumenyana na wenyeji Uruguay usiku wa manane.

Share This Article