Mashindano ya kutafuta mrembo atakayetangaza madini adimu ya Tanzanite kupitia jukwaa la Miss Tanzanite Manyara yanatarajiwa kufanyika usiku wa Novemba 16,2024 katika ukumbi wa kisora mjini Babati.
Mwaka huu mashindano hayo yamevutia washiriki zaidi ya 12 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania yametanguliwa na shindano la kusaka Top Model huku majaji watatu wakichuja na kutangaza warembo waliobobea kwa kuonesha vipaji vyao vya kuimba, ubunifu kwenye mavazi, kucheza na kuigiza katika hotel ya New Harambee.
Majaji wa mashindano hayo Eva Godwin, Mbaraka Sungi na Lucy Kimaro waliwatangaza Doreen Gasper, Jennifer Mmary na Jackline Kagila kuwa washindi katika suala la mavazi.
Washindi katika vipaji vya kucheza, kuimba na kuigiza ni Amina Ramadhani, Anelfaith Samwel na Rose Dickson.
Mshindi wa jumla atatangazwa siku ya Mashindano Novemba 16.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Natha’s Entertainment inayoandaa shindano hilo Aminatha Adolf Shamte, alisema tukio kubwa zaidi litafanyika Novemba 16, akitoa mwaliko kwa wananchi wafike kushuhudia mrembo akivishwa taji na wapate burudani.
Aminatha alisema mshindi wa shindano hilo atapeperusha bendera ya Manyara kote nchini Tanzania na nje katika kutangaza madini ya Tanzanite na vivutio vingine vilivyopo.