Sherehe za 61 za Mashujaa kaunti ya Kwale zanogesha biashara

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakazi wa kaunti ya Kwale wana kila sababu ya kutabasamu kutokana na sherehe za 61 za siku kuu ya Mashujaa zilizoandaliwa  Jumapili katika uwanja wa Kwale.

Biashara za iana mbalimbali zimenakili ongezeko la tija na faida kutokana na idadi  kubwa ya wageni na maafisa wa serikali waliofika kuhudhuria sherehe za mwaka huu.

Mikahawa,hoteli ,maeneo ya burudani na vyumba vya kulala vimenakili ongezeko la wateja katika kipindicha wiki moja iliyopita.

Kwenye hotuba yake wakati wa sherehe za leo Rais Ruto alisema  serikali yake iemtenga shilingi bilioni 1.5, kuanzisha mpango wa absentee landlords, kuwatafutia makao maskwota katika kaungti ya Kwale.

Ruto amewataka Magavana wa eneo la pwani kushirikiana na serikali kufanikisha  mpango wa kuwatafutia makao watu wasio na ardhi.

Share This Article