Shabana FC yatwaa taji ya taifa ya Super League

Tom Mathinji
2 Min Read
Timu ya Shabana yashinda timu ya NSL. Picha/Hisani

Timu ya soka ya Shabana, imetawazwa bingwa wa taji ya taifa ya Super League (NSL), baada ya kuiadhibu Kisumu All Stars mabao 2-0, katika mechi ya kusisimua iliyochezwa katika uwanja wa Gusii siku ya Jumamosi.

Nehemiah Onchiri’s aliiweka Shabana kifua mbele katika dakika ya 53, kabla ya kuongeza bao lingine katika dadika 83 na hivyo kutanyakua kombe hilo.

Shabana ambayo imekamilisha ligi hiyo ya Super ikiwa na alama 73, tayari ilikuwa imejikatia tiketi ya kujiunga na ligi kuu nchini, ikizingatiwa kuwa ingekamilisha ligi ya super ikiwa katika nafasi ya kwanza au ya pili. Timu ya Murang’a Seal pia imepanda ngazi na kupenya katika ligi kuu ya soka nchini, baada ya kumaliza ya pili katika Ligi ya taifa ya Super.

Kocha mkuu wa timu ya Shabana Sammy Okoth, aliimiminia sifa sufufu timu yake, kutokana na ushindi huo uliosubiriwa na hamu na ghamu.

“Tulitia bidii katika mechi zetu. Ilikuwa lazima tushinde mechi hii,”alisema kocha huyo.

‘Tore Bobe’ jinsi timu ya shabana inavyojulikana, awali ilitambulika kwa kuwa na wachezaji bora, ilishushwa kutoka ligi kuu ya taifa mwaka 2006, na kutamatisha kipindi cha miaka 21 katika ligi kuu.

Timu ya Shabana inahistoria nzuri ya soka hapa nchini, kwani ilisifika sana kwa kuwa na wachezaji wengi katika timu ya taifa ya soka Harambee stars katika miaka ya 80 na 90.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *