Police FC wanusia ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza

Police waliosalia na mechi dhidi ya Shabana na Gor Mahia, wanahitaji ushindi mmoja tu,kutawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Police FC wamejiweka katika nafasi bora ya kunyakua taji ya ligi kuu FKF, kwa mara ya kwanza baada ya kutanua pengo la pointi sita dhidi ya wapinzani wa karibu Tusker FC .

Maafande wamesajili ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Talanta FC, katika raundi ya 32 leo Jumapili huku wapinzani wao Tusker FC, wakiambulia kichapo cha kihistoria mabao 7-1 kutoka kwa Sofapaka, wakati mabingwa watetezi Gor Mahia wakitoka sare tasa na Muranga Seal.

Police FC walipata bao pekee na la ushindi kuanko dakika ya 15, kupitia kwa David Simiyu.

Police wanaongoza jedwali kwa alama 61,wakifuatwa na Tusker, kwa pointi 55 huku Gor, wakiwa na alama 54 katika nafasi ya tatu.

Kinyang’anyiro cha ubingwa wa msimu huu kinasalia baina ya Police, na Gor kwani Tusker, hata wakishinda mechi zote mbili wana uhaba wa magoli ya Police FC.

Police waliosalia na mechi dhidi ya Shabana na Gor Mahia, wanahitaji ushindi mmoja tu, ili kutawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza.

Gor nao waliosalia na mechi tatu dhidi ya Ulinzi,AFC Leoaprds na Police FC ni sharti washinde zote,  ili kuwa na fursa ya kutetea taji hiyo.

 

 

Website |  + posts
Share This Article