Karua na wenzake warejea nyumbani baada ya kuzuiwa kuingia Tanzania

Lissu amepangiwa kufikishwa mahakamani kesho Mei 19, kujibu mashtaka yanayomkabili ya uhaini na uchochezi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakili Martha Karua pamoja na mawakili wengine wa Kenya wamelazimika kurejea nyumbani baada ya kuzuiwa kuingia nchini Tanzania, kumwakilisha mteja wao Tundu Lissu ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye angalia anauziliwa gerezani.

Lissu amepangiwa kufikishwa mahakamani kesho Mei 19, kujibu mashtaka yanayomkabili ya uhaini na uchochezi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, amelaani hatua ya Serikali kumzuia Karua pamoja na Mawakili wengine wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki kuingia nchini kwa ajili ya kufuatilia kesi ya Lissu a.

Karua na Mawakili Gloria Kimani na Lynn Ngugi, walizuiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, mapema Jumapili punde walipowasili Dar.

Website |  + posts
Share This Article