Waziri Mvurya azindua kamati ya ukaguzi wa fedha

Kubuniwa kwa kamati hiyo kutahakikisha usimamizi bora wa fedha, kuwezesha uwajibikaji na uthabiti wa kifedha wa wizara hiyo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa masuala ya vijana, uchumi bunifu na michezo Salim Mvurya, amezindua kamati ya ukaguzi wa fedha za wizara hiyo inayoongozwa na Bi. Esther Muriithi Ndegwa.

Kubuniwa kwa kamati hiyo kutahakikisha usimamizi bora wa fedha, kuwezesha uwajibikaji na uthabiti wa kifedha wa wizara hiyo.

Akizungumza leo Jumatano alipozindua kamati hiyo katika jumba la Talanta, Waziri Mvurya, alikariri kujitolea kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha wanazotengewa na serikali kuu.

Kuhusu madeni ya wizara hiyo ambayo hayajalipwa, Mvurya aliema yalitokana na maamuzi duni katika usimamizi wa miradi na kukosa kutekeleza mapendekezo ya wakaguzi wa fedha.

Aidha, waziri ameitaka kamati hiyo kuinua viwango vya uchunguzi , ukaguzi na usimamizi bora wa fedha katika Wizara hiyo.

Website |  + posts
Share This Article