Serikali yapunguza karo ya Vyuo Vikuu vya Umma

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali yapunguza karo ya vyuo vikuu vya umma.

Serikali imepunguza karo ya vyuo vikuu vya umma, katika hatua inayonuiwa kuwapunguzia wanafunzi na familia zao mzigo.

Kulingana na katibu wa Elimu ya Juu Dkt. Beatrice Inyangala, hatua hiyo imetokana na mashauriano ya kina na wanafunzi, umma na wadau wa Elimu ya Juu.

Alisema mabadiliko hayo yanazingatia mfumo wa ufadhili wa wanafunzi, unaohakikisha kuwa karo hiyo inagawanywa kupitia ufadhili mbali mbali wa serikali, mikopo ya wanafunzi na mchango wa familia kulingana na mahitaji.

“Hatua hii ya kijasiri inaashiria kujitolea kuhakikisha elimu ya vyuo vikuu ambayo ni nafuu, inayopatikana na yenye ubora wa hali ya juu, huku udhabiti wa kifedha wa taasisi zetu ukidumishwa,” alisema Dkt. Inyangala.

Vyuo vikuu vya Umma vimeagizwa kutekeleza mfumo huo mpya wa karo kufikia Septemba 1, 2025, kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo.

Dkt. Inyangala alirejelea kwamba mabadiliko hayo ya hivi punde, ni sehemu mpana wa serikali kufanyia marekebisho sekta ya elimu ya juu kuwa nguzo ya maendeleo ya taifa.

Website |  + posts
Share This Article