Mudavadi: Kenya itaendelea kukuza uhusiano wake na Serbia

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi amkaribisha hapa nchini Mama taifa wa SerbiaTamara Vučić.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu aliye pia waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi, leo Jumamosi alikuwa mwenyeji wa Mama wa taifa wa Serbia Tamara Vučić, tanayezuru hapa nchini kwa shughuli rasmi.

Wawili hao walishiriki mazungumzo yaliyolenga kuimarisha uhusiano uliodumu kwa miaka mingi baina ya mataifa hayo mawili.

“Tuliangazia fursa mpya za kukuza ushirikiano dhabiti, ambao umedumu kwa miaka mingi,’ alisema Mudavadi.

Mudavadi aliishukuru Serbia kwa kusimama na Kenya na kusaidia taifa hili lilipoathiriwa na mafuriko kwa kutoa msaada wa yuro 150,000, kusaidia katika utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa jamii zilizoathiriwa.

“Kenya imejitolea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, hususan kupitia sekta za biashara, elimu, Teknolojia ya habari na mawasiliano miongoni mwa zingine,” alidokeza waziri huyo.

Website |  + posts
Share This Article