Serikali yalenga kuangamiza malaria kufikia 2030

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali imeweka mpango kabambe unaolenga kuangamiza kabisa ugonjwa wa malaria nchini kufikia mwaka 2030.

Maambukizi ya ugonjwa huo nchini kwa sasa ni asilimia 6.

Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni anasema serikali kwa sasa inasambaza neti milioni 15 katika kaunti 22 ambazo zinakabiliwa na hatari kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria.

Hii ni sawa na Wakenya wapatao milioni 25 walio katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Muthoni aliyasema hayo wakati akiongoza kampeni ya usambazaji neti kwa kaya zipatazo 200,000 katika kaunti ya Kilifi.

Aliongeza kuwa hadi kufikia sasa, kaunti 14 zimenufaika na mpango huo.

Aidha, amedokeza kuwa serikali itaanzisha kampeni ya kuwaelimisha Wakenya kuhusiana na namna ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira wanamoishi.

Katika kaunti ya Kilifi, serikali inalenga wakazi wapatao milioni 1.9.

Naibu Gavana wa kaunti hiyo Flora Mbetsa Chibule anasema serikali ya kaunti inalenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa asilimia 50.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *