Azimio ndio yenye wabunge wengi, yaamua Mahakama Kuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama Kuu imeamuru kuwa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, ndio wenye idadi kubwa ya wabunge katika Bunge la Taifa na wala sio muungano wa Kenya Kwanza.

Kwenye uamuzi huo wa kihistoria uliotolewa leo na majaji John Chigiti, Jairus Ngaah, na Lawrence Mugambi, wamebatilisha uamuzi wa Spika Moses Wetang’ula, aliyesema kuwa muungano wa Kenya Kwanza ndio uliopata wabunge wengi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Ken Njagi, wakili Lempaa Soyinka, na watu wengine 10 waliowakilishwa na wakili Kibe Mungai.

Licha ya Wetang’ula kusema kuwa wabunge 14 kutoka vyama vinne vya muungano wa Azimio walikuwa wamemwandikia barua ya kujiondoa katika muuungano huo, alishindwa kutoa ushahidi huo mahakamani.

Uamuzi huo unatarajiwa kuathiri nafasi kadhaa za uongozi katika Bunge la Taifa, ikiwemo viongozi wa walio wengi na wachache na pia viranja wa wengi na wachache.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *