Serikali pamoja na washirika wa kimaendeleo, wamebuni jopo kazi litakaloshughulikia kwa haraka matumizi ya fedha za ufadhili zilizotengewa mipango mbali mbali kote mchini.
Pia watamarisha uwezo wa taifa hili katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na changamoto zinazotatiza ustawi wa kiuchumi na kijamii wa taifa hili.
Naibu Rais Rigathi Gachagua, alisema kubuniwa kwa jopo kazi hilo ni sehemu ya hatua ambazo zimechukuliwa na utawala wa Kenya Kwanza kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na washirika wa kimaendeleo na kuchochea ukuaji wa kijamii na kiuchumi.
“Tunahimiza ushirikiano na washirika wetu wa kimaendeleo….tumeondoa vikwazo vinavyodumaza ushirikiano huo. Rais ameelezea haja ya kurahisisha hatua za ushirikiano,” alisema Gachagua.
Gachagua aliyasema hayo leo Jumanne, katika kikao cha pili cha washirika wa kimaendeleo katika makazi yake rasmi ya Karen.
Akizungumza katika mkutano huo, mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, alisema kikao hicho kinadhamiria kuimarisha ushirikiano katika mipango ya maenedeleo kwa taifa hili.
Aidha, aliwaambia mawaziri, mabalozi, maafisa wa ngazi za juu wa serikalini na wawakilishi wa mashirika mbali mbali kwamba rais Ruto amejitolea kuhakikisha kuwa serikali inatimiza wajibu wake kwa Wakenya.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wenyekiti wenza wa kikao hicho ambao ni Sebastia Tebastian Groth (Balozi wa Ujerumani nchini Kenya) na Dkt. Stephen Jackson (Mshirikishi wa shirika la Umoja wa Mataifa.
Wengine ni pamoja na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, Cabinet Secretaries, Mabalozi, maafisa wa ngazi za juu serikalini na wawakilishi wa mashirika mbali mbali.