Serikali ya kaunti ya Nyandarua yahimizwa kutumia vituo vya huduma kwa wakulima

Marion Bosire
1 Min Read

Serikali ya kaunti ya Nyandarua imehimizwa kutumia vituo vilivyopo vya huduma kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na faida ya mazao ya shamba.

Akizungumza waati wa kikao cha mafunzo kwa mameneja wa vituo hivyo vya huduma kwa wakulima, Fredrick Opondo kutoka kwa chama cha wakulima wa nafaka alisema kwamba iwapo vituo hivyo vitatumiwa, wakulima watapata huduma za ushauri wa kitaalamu, mafunzo na mbinu za kisasa za kilimo, vitu ambavyo ni muhimu kwa kilimo endelevu.

Kulingana naye, vituo hibyo hufanikisha pia vipimo vya udongo, mbinu za kupambana na wadudu na magonjwa, wakulima wanaweza kupata mbegu bora, mbolea na hata kuunganishwa na masoko ya mazao yao.

Margret Wamithi kutoka KUZA alikuwa na maoni sawia ambapo aliongeza kwamba wakulima watakapoanza kutumia mbinu bora na kuongeza mazao faida itakuwa kubwa kwa mfumo wote wa uchumi katika eneo husika.

Wamithi alisema mafunzo hayo ya wiki 15 yanalenga kuwapa mameneja wa vituo vya huduma kwa wakulima ujuzi na vifaa vinavyohitajika ili kuhudumia wakulima na kuwahimiza watumie raslimali zilizopo.

Mameneja hao wanahisi kwamba mafunzo wanayopokea yatawasaidia katika kutekeleza kazi zao nyanjani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *