Serikali imejipata njia panda baada ya mahakama kusimamisha zoezi la kitaifa la usajili wa makurutu wa polisi kiwango cha Constables, iliyokuwa imeratibiwa kuanza leo Ijumaa.
Jaji Hellen Wasilwa wa mahakama ya Milimani alitoa uamuzi huo jana kwenye kesi iliyowasilishwa na mbunge wa Kilome Harun Mwau.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 21 mwezi huu.
Usajili huo ulikuwa ufanyike katika vituo 416 katika kaunti zote 47 nchini baina ya leo na tarehe 9 mwezi huu.