Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amezindua bodi ya kuimarisha uzalishaji mifugo katika hatua inayolenga kupiga jeki sekta ya mifugo nchini.
Akihutubu baada ya kuzindua bodi hiyo, Kagwe amesema ataunga mkono kikamilifu bodi hiyo itakayotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia mfumo wa mabadiliko ya kiuchumi wa serikali wa kuanzia chini hadi juu (BETA).
Waziri ameitaka bodi hiyo kupanua uwekezaji katika sekta ya mifugo, ambayo ni asilimia 90 ya kitega uchumi kwa familia za maeneo kame, na pia hutoa nafasi za ajira kwa asilimia 95.
Waziri huyo aliangazia miradi kama vile kiwanda cha ngozi cha Kenanie na kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo kwa mifugo kuwa chachu muhimu katika kuimarisha sekta ya ufugaji.