Seneti yatupilia mbali hoja ya kumtimua Gavana Mutai

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Kericho Eric Mutai.

Ni afueni kwa Gavana wa kaunti ya Kericho Eric Mutai, baada ya bunge la Seneti leo Jumatatu kutupilia mbali hoja ya kumuondoa mamlakani.

Maseneta 34 walipiga kura, kusimamisha vikao kwa kusikiliza hoja ya kumbandua Mutai.

Huku wakipinga hoja hiyo, Maseneta hao walisema bunge la kaunti ya Kericho halikuafikia hitaji la thuluthi mbili kuunga mkono kuondolewa kwa Gavana huyo.

Mutai alikabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo; ukiukaji wa katiba, ufujaji wa fedha za umma, uteuzi usio halali na utumizi mbaya wa mamlaka.

Makosa mengine yalijumuisha uchochezi na dhuluma za kijinsia.

Hata hivyo, Gavana Mutai alikanusha mashtaka hayo, yaliyowasilishwa katika bunge la Senate na bunge la kaunti ya Kericho.

TAGGED:
Share This Article