Serikali ya Kenya Kwanza iliafikia ufanisi mkubwa mwaka huu katika sekta mbalimbali.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Msemaji mkuu wa serikali Isaac Mwaura ametaja baadhi ya mafanikio hayo kama ongezeko la watalii kutoka milioni 1.48 mwaka jana hadi milioni 2.5.
Mavuno ya wakulima pia yaliongezeka kutokana na hatuabya serikali kupunguza bei ya mbolea kutoka shilingi 7,500 hadi 2,500, hali iliyochangia kuongezeka kwa mazao yaliyochangia wakulima kuvuna magunia milioni 95 ya mahindi,magunia milioni 10 ya ngano na magunia milioni 2 ya mpunga.