Ruto: Kindiki kutoa huduma nilizokosa kwa miaka miwili

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema ana imani na Naibu Rais Kithure Kindiki kuwa ataboresha utendakazi wa serikali yake katika manifesto ya Kenya Kwanza.

Akihitubu katika ukumbi wa KICC baada ya Kindiki kula kiapo cha utendakazi, Ruto amesema amekuwa akikosa mtu wa kuuza sera za serikali katika Baraza la Mawaziri na pia kwa Wakenya kuhusu ajenda za serikali kwa miaka miwili iliyopita.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Ruto kuzungumzia utendakazi wa aliyekuwa Naibu wake Rigathi Gachagua aliyetimuliwa na utendakazi wake.

“Nimekuwa pekee nikizungumzia kuhusu ajenda ya serikali katika Baraza la Mawaziri na kwa Wakenya ikiwemo nyumba za gharama nafuu na mfumo mpya wa ufadhili wa elimu.Nnina imani profesa una tajriba na uwezo wa kunipa msaada ambao nimekosa kwa miaka miwili iliyopita,”akasema Rais Ruto.

Kindiki anatwaa mikoba ya Naibu Rais akiwa wa tatu kuhudumu katika afisi hiyo baada ya Rais William Ruto na Gachagua.

Website |  + posts
Share This Article