Samuel Eto’o aadhibiwa na CAF kwa ukiukaji maadili

Tom Mathinji
1 Min Read
Samuel Eto'o

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), limemtoza faini ya $200,000 rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto’o, kwa ukiukaji wa maadili, lakini ikapata ushahidi wa kutosha kuendelea na mashtaka yanayohusiana na madai ya upangaji matokeo.

Shirikisho hilo la Soka Afrika, lilianzisha uchunguzi kuhusu mwenendo wa Eto’o mwezi Agosti mwaka jana baada ya kupokea “taarifa zilizoandikwa kutoka kwa wadau kadhaa wa soka wa Cameroon”.

Jopo la nidhamu lilibaini kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika mara nne “amekiuka kwa kiasi kikubwa kanuni za maadili, uadilifu na uanamichezo” za Caf kwa kutia saini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya kamari ya 1XBET.

Mawakili wa Eto’o wamesema watakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *