Samia afanya mageuzi ya Wakuu wa Mikoa, awateua wanne wapya

Kwenye mabadiliko hayo, Rais Suluhu aliwahamisha Wakuu wa mikoa sita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Samia Suluhu wa Jamhuri ya Tanzania siku ya Alhamisi alifanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa huku akiwateua wengine wanne wapya walioshindwa kwenye uchaguzi kwa tiketi ya chama cha CCM.

Kwenye mabadiliko hayo, Rais Suluhu aliwahamisha Wakuu wa Mikoa sita.

Mbunge wa zamani wa Misungwi, Alexander Mnyeti aliteuliwa Mkuu mpya wa mkoa wa Geita huku mbunge wa zamani wa Maswa Mashariki Stanlaus Nyongo, akiteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

 

Share This Article