Bingwa wa Olimpiki Faith Cherotich alifunga msimu wa Diamond League kwa njia ya kipekee, akipata ushindi katika mkondo wa 14 wa Zurich Alhamisi usiku.
Cherotich a,ishinda mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa kutumia dakika 8 sekunde 55.82, na kufuzu kwa fainali ya Brussels wiki ijayo.
Mkenya mwenza Dorris Lemngole alichukua nafasi ya pili kwa dakika 8 sekunde 57.89,sekunde 0.12 nyuma ya Cherotich.
Bingwa wa zamani wa Olimpiki Peruth Jemutai wa Uganda,aliambulia nafasi ya tatu.
Cherotich anajiandaa kwa mkondo wa fainali wa Diamond League utakaoandaliwa Septemba 4 na 5 mjini Brussels,Ubelgiji.

Bingwa wa Olimpiki na Dunia Emmanuel Wanyonyi, alishinda mita 800 ambazo hazikuwa za kuwania pointi,kwa kuweka muda bora wa dakika 1 sekunde 41.76,akifutwa na Djamel Sedjaati wa Algeria, huku Slimane Moula pia kutoka Algeria akichukua nafasi ya tatu.
Phanuel Kosgei alichukua nafasi ya pili katika mita 1500,akitumia dakika 3 sekunde 31.84, nyuma ya Cole Hocker wa Marekani, aliyeshinda kwa dakika 3:31.74.
Aliyekuwa bingwa wa Dunia mwaka 2019,Timothy Cheruiyot alimaliza wa 11.