Waganda wahaha Mfalme Oyo akiwa si maji wala uji

Mfalme Oyo alishika hatamu akiwa na umri wa miaka mitatu, akiwa Mfalme mwenye umri mdogo zaidi kote ulimwenguni.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mtafaruku na hofu kubwa imetanda katika Ufalme wa Tooro nchini Uganda baada ya kutangazwa kuwa Mfalme Oyo Kabamba Iguru Rukidi wa nne yumo katika hali mahututi.

Kupitia kwa taarifa ya ukurasa wa X iliyochapishwa na Waziri Mkuu (Omuhikirwa), Calvin Armstrong Rwomiire Akiiki, Mflame huyo aliye na umri wa miaka 34 alishika utawala mwaka 1995, akimrithi babake Mfalme Patrick David Kaboyo Olimi 3.

Waziri Mkuu aliwataka Waganda kumwombea Mfalme huku akiwataka kuepuka kueneza habari za porojo, akisistiza kuwa watatoa taarifa kamili.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Waganda kumwombea Mfalme.

Mfalme Oyo alishika hatamu akiwa na umri wa miaka mitatu, akiwa Mfalme mwenye umri mdogo zaidi kote ulimwenguni.

Share This Article