Utawala wa Kenya Kenya Kwanza utawahudumia Wakenya wote bila upendeleo wowote.
Rais William Ruto anasema kila sehemu ya nchi ni muhimu na itahudumiwa na serikali yake bila kujali namna wakazi wa sehemu hizo walivyopiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
“Tutawahudumia Wakenya kwa usawa. Wale waliotupigia kura na wale ambao hawakutupigia kura,” aliahidi Rais Ruto wakati wa kuapishwa kwa Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki.
Rais alisisitiza kuwa Kenya ni nchi moja bila kujali wanakoishi Wakenya na kuonya dhidi ya uenezaji wa ukabila.
Ruto alimtaka Prof. Kindiki kuwahudumia Wakenya bila upendeleo, uoga wala nia mbaya akielezea imani kuwa atamsaidia kueneza injili ya miradi inayotekelezwa na serikali.
Matamshi hayo yalionekana kuwa vijembe alivyoelekezewa Naibu Rais aliyebanduliwa madarakani Rigathi Gachagua.
Gachagua alinukuliwa akisema Wakenya watapata huduma za serikali kulingana na jinsi walivyopiga kura.